Na: Nassoro Rashid
MDC Habari
Halmashauri ya wilaya ya Mkinga kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu kwa kushirikiana na wadau wa shirika la World Vision wametoa semina kwa wanaume kuhusu ushiriki wao katika unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto.
Semina hiyo imetolewa leo Agosti 07, 2023 katika ukumbi mdogo wa Shirika la World Vision uliopo wilayani humo ikiwa ni katika kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kwa wanaume wenye watoto walio katika umri wa kunyonya ambao ni chini ya miaka miwili (2).
Awali akifungua semina hiyo Mganga Mkuu wa wilaya Dkt. Joseph Ligoha ameeleza kwa upana faida za unyonyeshaji kwa mama na mtoto
zikiwemo kumuepusha mama na hatari ya kupata saratani pamoja na kumsaidia mtoto kukua vizuri kiafya na kiakili.
"Semina hii imelenga kuwafundisha wanaume namna ya kuwajibika katika kusaidia wanawake wanaonyonyesha waweze kupata muda mzuri na mazingira rafiki ya kunyonyesha watoto ili waweze kukua vizuri kiafya". alisema Dkt. Ligoha
Ifahamike kuwa maadhimisho ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mtoto Duniani yalianza tangu Agosti 01, 2023 na kuhitimishwa leo tarehe 07.08.2023 ikiwa na kauli mbiu ya "Saidia Unyonyeshaji, Wezesha Wazazi kulea Watoto na Kufanya kazi zao kila Siku".
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 027-2660501
Simu: +255 684 625 299
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017