Na: Nassoro Rashid - Mkingadc Habari
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Mhe. Amani Juma Kasinya Agosti 20, 2024 ameongoza Mkutano wa Baraza Maalum la Madiwani wa kupitisha mapendekezo ya Rasimu ya Sheria ndogo za Uhifadhi wa Bahari (BMU) uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Baraza hilo maalum lililodhaminiwa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network ambao pia ndio waliodhamini mchakato wa upatikanaji wa sheria hizi tangu mwanzo mpaka kufikia hapa.
Kupitia Mkutano huo Mhe. Kasinya amesema kwa kushirikiana pamoja na Madiwani wamefanikiwa kupitia na kujadili kwa kina Rasimu ya sheria hiyo kutoka katika Kata tatu (3) zinazohusisha vijiji saba (7) ikiwemo Kijiji cha Moa, Kwale, Mongaveru, Bomasubutuni, Bomakichakamiba, Zingibari na Mwaboza.
Ifahamike kuwa mchakato huo wa sheria za usimamizi wa Bahari mpaka kufikia leo kujadiliwa na Baraza hilo ni mara baada ya kujadiliwa na kupita kuanzia ngazi ya Serikali ya Vijiji, Kata, Kamati ya Wataalam, Kamati ya Fedha hadi Baraza.
#Kaziiendelee
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 027-2660501
Simu: +255 684 625 299
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017