1.0 UTANGULIZI
Wilaya ya Mkinga ni mojawapo ya Wilaya nane za Mkoa wa Tanga ambayo ilianzishwa rasmi tarehe 01/07/2006 baada ya kugawanywa kutoka Wilaya ya Muheza. Wilaya hii imepakana na Wilaya za Muheza na Tanga kwa upande wa Kusini, Wilaya za Korogwe na Lushoto upande wa Magharibi, Jamhuri ya Kenya upande wa Kaskazini na Bahari ya Hindi upande wa Mashariki,Wilaya iko kati ya Latitude -4.7952766 na Longitude 38.904164
2.0 MUUNDO WA UTAWALA
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ilianzishwa rasmi tarehe 1.7.2017 inazo Tarafa 2, Kata 22, Vijiji 85 na Vitongoji 335 Kwa Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Mkinga ilikuwa na Jumla ya wakazi 118,065, kati yao Wanawake walikuwa 60,305 na Wanaume 57,760 . Aidha kwa kuzingatia ongezeko la watu la asilimia 1.27 Wilaya ina idadi ya watu 127,352 kati yao Wanaume 62,303 na Wanawake 65,049 kwa mwaka 2017.
3.0 HALI YA HEWA
Wilaya iko kwenye mwinuko wa mita 192 sawa na futi 630 kutoka usawa wa bahari na hali ya joto ni Wastani wa joto ni nyuzi 24ºC hadi 28ºC wakati wa baridi (Desemba-Machi) na wakati wa joto (Mei – Oktoba) kati ya nyuzi 29ºC hadi 30ºC. Wilaya ina misimu miwili ya mvua: Mvua za vuli na Mvua za Masika. Mvua hizo hunyesha kwa wastani wa kati ya milimita 400 hadi 1,400 kwa mwaka.Pia hupata wastani wa mvua wa 800-1000 mm kwa mwaka. Aina kuu za udongo zinazopatikana ni tifutifu (loamy), mfinyanzi – tifutifu (clay-loamy) na kichanga (sand).
ORODHA YA WAKURUGENZI
No |
Jina kamili |
Mwaka alioanza |
Mwaka alioondoka |
1 |
Philbert Sebastian Ngaponda |
2007 |
2012 |
2 |
Amina Kiwanuka |
2012 |
2016 |
3 |
Emanuel Mkumbo |
2016 |
2016 |
4 |
Rashid Karim Gembe |
2017 |
2021 |
5 |
Zahara Abdul Msangi |
2021 |
Mpaka sasa |
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 755 443 326
Simu: +255 755 443 326
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017