Na: Nassoro Rashid - Mkinga DC Habari
Wilaya ya Mkinga yaadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa leo Julai 25, 2024 kwa kufanya usafi katika eneo la Hospitali ya Wilaya.
Zoezi hilo la usafi limeongozwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Ndugu Palango Salum Abdul kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Rashid Karim Gembe.
Sambamba na hayo makundi mbalimbali yameshiriki katika zoezi hilo la Usafi yakiwemo Watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi, Takukuru, Jeshi la Wananchi, Magereza, Uhamiaji, Jeshi la Akiba pamoja na viongozi wa Kata ya Parungu Kasera, Kijiji cha Kasera na Wananchi.
#Kaziiendelee
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 027-2660501
Simu: +255 684 625 299
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017