• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mkinga District Council
Mkinga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Livestock and Fishary
      • Works and Fire Recure
      • Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari Mawasiliano na Uhusiano
      • Ugavi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Legal
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma wa Maji
    • Huduma ya Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Maktaba ya Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Matukio
    • Habari
    • Matukio

MKUU WA WILAYA YA MKINGA AMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTEKELEZAJI MZURI WA AFUA ZA LISHE KWA NGAZI YA KATA YA WILAYA

Posted on: December 7th, 2023

Na: Nassoro Rashid - MDC Habari

Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mhe. Kanali Maulid Hassan Surumbu Disemba 07, 2023 amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Zahara Msangi kwa utekelezaji mzuri wa afua za lishe kwa ngazi ya Kata na Wilaya.

Akizungumza wakati wa kikao cha kutathmini utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa robo ya kwanza Mhe. Surumbu amesema Wilaya kwa sasa ipo vizuri katika utekelezaji wa afua hizo kwa kulinganisha na robo iliyopita.

"Matokeo ya hali ya lishe kupitia kadi alama ya robo ya kwanza inaonesha ni kiasi gani dhana ya ushirikishwaji kuanzia ngazi ya chini hadi juu imeetekelezwa ipasavyo, hakika tukiendelea na utaratibu huu naamini tutazidi kuwa pahala pazuri zaidi, na hii inaonesha kuwa kila mtendaji wa kata amefanya kazi yake vizuri, hivyo nampongeza sana Mkurugenzi na timu yake kwa kusimamia utekelezaji huu". Alisema Mhe. Surumbu.

Kadhalika Mhe. Surumbu ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Mkinga kuendelea kuwaunga mkono viongozi katika utekelezaji wa afua za lishe kuanzia ngazi ya Kijiji, Kitongoji, Kata mpaka Wilaya ili kuimarisha ongezeko la uelewa wa umuhimu wa lishe kwa watoto na jamii kwa ujumla.

Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza Watendaji wa Kata kwa kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali huku akiwataka kuongeza pia juhudi zaidi na maeneo mengine ikiwemo ufuatiliaji na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kuukuza uchumi wa wana Mkinga.

Ifahamike utekelezaji wa afua za lishe umekuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa maendeleo kwa jamii hivyo Wananchi wanaendelea kuhimizwa kuweka kipaumbele kwenye utekelezaji wa afua mbalimbali nchini ili kuwezesha kuwa na Taifa lenye watu wenye afya na lishe bora ili kufikia malengo endeleevu.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA October 16, 2023
  • HATI MILIKI ZA ARDHI ZILIZOKAMILIKA WILAYA MKINGA December 04, 2022
  • KUSAFISHA MAENEO KWA WAMILIKI WA VIWANJA MKINGA August 12, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA July 18, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WITO WATOLEWA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA, MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA NA ULAWITI (W) MKINGA

    August 21, 2024
  • JAMII YAASWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA HOMA YA NYANI WILAYA YA MKINGA

    August 20, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA MAALUM LA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA SHERIA NDOGO ZA UHIFADHI WA BAHARI (BMU)2024

    August 20, 2024
  • BARAZA LA MADIWANI, MKURUGENZI MTENDAJI, WATAALAM NA WATUMISHI WOTE WANAKUKARIBISHA MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLAH HALMASHAURI YA (W) MKINGA

    August 16, 2024
  • Angalia Zaidi

Video

Angalia zaidi

Kurasa za Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Habari

Kurasa Mashuhuri

  • OR- TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Salary slip portal
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Taifa
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Kasera, Tanga -HorohoroRoad

    Postal Address: P O Box 6005 Tanga

    Simu: +255 027-2660501

    Simu: +255 684 625 299

    Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Huduma

Mkinga dc @ 2017