Pichani aliesimama ni Mh Mkuu wa Wilaya Kanali Maulid Hassan Surumbu, akisisitiza jambo kwenye Mkutano mkuu wa Kata katika Kata ya Kwale.
Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata wakiwemo viongozi wa chama na serikali lengo ;likiwa ni kuwapongeza wananchi wa kata ya kwale kwa kukusanya mapato vizuri na kuisaidia Wilaya kufikia asilimia 80% na kuitanga kuongeza walau kufikia alisimia 90 na zaidi. mapato mengi katikaukana wa pwani hasa kata ya Kwale na Nyingine husababisha=wa hasa na kilimo bahari pamoja na Uvuvi.
pamoja na changamooto mbalimbali zinazoikabili sekta ya uvuvi pia Mh Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wa Kwale kuepuka kushiriki uvuvi haramu hasa ule wa kutumia mabomu na nyavu zisizofaa.
mwisho aliwahasa wananchi wa Mkinga kwa ujumla juu ya Ulinzi shirikishi hasa katika jamii yetu na kuwataka kutambua kwamba " wanaojihusisha na uvuvi haramu, matumiziu ya nyavu zisizofaa na hata wizi ni ndugu zete, watoto wetu, marafiki zetu hivyo basi nawahasa kuanza kuambiana na kukanyana wenyewe kwa wenyewe ili mwisho wa nsiku tusije kulaumiana"
mwisho aliwatakia wanakwale amani na mshikano uliopo uendelee na kuepuka kupokea wageni hasa tusiowajua wanaotumia bahari kuja kwetu na kama utamuona jitahidi kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi vinavyohusika.
Baadhi ya wananchi ambao ni wavuvi na Wakulima wa Mwani pamoja Viongozi wa Kata ya Kwale waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Kata ya Kwale.
Aliesimama ni Mh. Diwani Kata ya Kwale akizungumza jambo katika Mkutano Ktika kata ya Kwale.
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 027-2660501
Simu: +255 684 625 299
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017