Na: Nassoro Rashid - MDC Habari
Kauli hiyo imesemwa Disemba 9, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Kanali Maulid Hassan Surumbu wakati akihutubia Wananchi katika maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru kiwilaya yaliyofanyika katika Ukumbi uliopo makao makuu ya ofisi za Halmashauri.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mhe. Surumbu amesema kuna kila sababu ya kuendelea kuuenzi uhuru wa nchi yetu kulingana na maendeleo mbalimbali yaliyofikiwa kupitia awamu mbalimbali za viongozi tangu mwaka 1961 hadi sasa huku akielezea kuwa wilaya ya Mkinga ilikuwa na mchango katika kupigania uhuru huo.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametanabaisha kwamba serikali ya wilaya ya Mkinga kwa kushirikiana na Wananchi imepiga hatua ya maendeleo katika miaka 62 kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kabla ya uhuru haikuwepo.
"Miaka 62 ya Uhuru Wilaya ya Mkinga imepiga hatua ya maendeleo katika nyanja tofauti ikiwemo sekta ya afya, kabla ya uhuru hatukuwa na vituo vya afya lakini sasa tunavyo 43, tulikuwa na shule za msingi 15 na sasa tunazo 85, hatukuwa na shule za sekondari lakini sasa tunazo 17, kadhalika sekta ya kilimo kumekuwa na ongezeko la mazao ya korosho, mkonge na viungo, pia tumepiga hatua sekta ya nishati ambapo Mkinga kwa sasa inapokea umeme kutoka gridi ya Taifa". Alisema Mhe. Kanali Surumbu.
Sambamba na hayo Mhe. Surumbu ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuilinda amani na mshikamano uliopo huku akiwataka vijana kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia fursa zilizopo kuiletea zaidi maendeleo wilaya ya Mkinga.
Maadhimisho hayo yaliohudhuriwa na makundi mbalimbali ya watu ikiwemo kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wazee maarufu waliokuwepo kipindi cha Uhuru, Watumishi, Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari pamoja na Wananchi yamekuwa ni sehemu ya kuhitimisha sherehe hizo mara baada ya shughuli mbalimbali kufanyika tangu Disemba 1, 2023 ikiwemo kufanya usafi wa Mazingira, Bonanza la Michezo, Mashindano ya uandishi wa Insha kwa Wanafunzi pamoja na upandaji wa miti.
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 755 443 326
Simu: +255 755 443 326
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017