Pichani aliesimama ni Mh. Mkuu wa Wilaya Mkinga Kanali Maulid Hassan Surumbu akizungumza na wananchi wa Kata ya Mayomboni wanaojihusisha na Uvuvi pamoja na kilimo bahari..
Mh. Mkuu wa Wilaya Mkinga Kanali Maulid Hassan Surumbu, Amehitimisha rasmi ziara yake kaliokuwa akiifanya katika Tarafa ya Mkinga kwa kuzungumza na Wananchi wanaojishughulisha na uvuvi pamoja na kilimo bahari leo katika Kijiji cha mayomboni ambapo amewataka wananchi hasa wanaotumia maeneo ya bahari kuacha kujihusisha na vitendo haramu kama vile kusafirisha wahamiaji haramu, madawa ya kulevya sambamba na uvuvi haramu kwa kutumia zana za uvuvi zisizofaa.
lengo la mkutano huu ni kuwapongeza Wananchihasa katika sekta ya uvuvi kwa kazi nzuri ya kuinua Mapato ya halamashauri hadi kufikia 88%, na kuwataka kuongeza uzalishaji ili kuweza kufikia asilimia 99% ya mapato ya Wilaya.
Pia Mh. Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi hao kuzungumza na watu wanaojihusisha na vitendo haramu akiamini kuwa watu hao hawatoki mbali na hapo ni baadhi ya ndugu, jamaa na marfiki zetu hivyo waambieni kwani kitakachokuja kuwapata wasije wakailamu serikali.
Aliesimama kulia ni Bi. Asha Churu ambae ni Kaimu Mkurugenzi na pia nI Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi wa Wilaya akifafanua jambo katika Mkutano huo/.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye Mkutano wakiwemo wavuvi na wakulima wa zao la mwani.
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 027-2660501
Simu: +255 684 625 299
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017