Na: Nassoro Rashid - Mkingadc Habari
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mhe. Husna Juma Sekiboko aridhishwa na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa wilayani Mkinga.
Ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya kutembelea wilaya 9 za mkoa wa Tanga Julai 08, 2024 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake aliojiwekea kusikiliza changamoto za Wananchi anaowawakilisha, kutembelea miradi pamoja na kuimarisha ujenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
"Hii ni wilaya yangu ya tisa katika ziara yangu hii ambapo leo nahitimisha kwa kufanikisha kupita kila Tarafa, hapa Mkinga nilianza Maramba na leo ni tarafa ya Mkinga, katika maeneo yote niliyopita nimeshuhudia miradi mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, maji, biashara, barabara, ambayo inagusa maendeleo ya Mwananchi wa Tanzania, hakika haya ndio maendeleo tunayoyataka". Alisema Mhe. Sekiboko
Aidha Mhe. Sekiboko ameipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushusha fedha nyingi katika Halmashauri zote za mkoa wa Tanga na kufanikisha kutekeleza miradi hiyo.
"Nimeshuhudia vituo vya afya vingi, zahanati na hapa Mkinga nimeshuhudia hospitali ya wilaya yenye majengo mazuri
na yanavutia, bado mengine yanaendelea kujengwa, inaonesha kwa kiasi kikubwa thamani ya fedha imeendana na thamani ya mradi, niwapongeze viongozi wote na wataalamu kwa kusimamia utekelezaji huu". Aliongezea Mhe. Sekiboko
Kadhalika Mbunge huyo amewaomba viongozi pamoja na wataalamu kuendelea kumsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kwa kutatua changamoto zao na kusimamia utekelezaji wa sera kwa vitendo ili kuendelea kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi yetu.
Pamoja na hayo ziara hiyo imekuwa na tija kwa Mhe. Sekiboko hususani katika kuendelea kuhamasisha Wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwa kuwa tayari kushiriki katika uandikishaji wa daftari la
mpiga kura lililoboreshwa utakapoanza na uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
#Kaziiendelee
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 027-2660501
Simu: +255 684 625 299
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017