Wilaya ya Mkinga ambayo haina hospitali ya Wilaya yenye vituo vitatu vya Afya ambavyo ni Mjesani, Maramba na Kiwegu. Kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea kupata huduma za upasuaji katika Hospitali ya Mkoa Bombo. Ukosefu wa huduma ya upasuaji katika vituo vya afya imekua adhaa kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Mkinga wanaokadiriwa kufika 118,065 kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Pia ukosekanaji wa huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito imekuwa ikisababisha vifo na matatizo mbalimbali ya uzazi kwa akina mama kwa kuwa ilihitajika kumsafirisha mgonjwa hadi Hospitali ya Rufaa Bombo ili kupata matibabu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga iliazimia kuanza kuvijengea uwezo vituo vyake vya Afya ili viweze kutoa huduma ya upasuaji kwa kuanza na kituo cha Afya Maramba. Uboreshaji wa kituo cha Afya Maramba ulianza kwa kuongeza eneo la kituo, Ujenzi wa Chumba cha Upasuaji, kukukarabati miundombinu ya kituo, Ununuzi vifaa tiba pamoja na kuongeza wataalum mbalimbali wa kada ya afya ili kufikia viwango vinavyokubalika.
Baada ya kumalizika kwa uboreshaji wa kituo cha Afya Maramba mnamo tarehe 21/07/2017, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ndugu Rashid K. Gembe alikadhi miundombinu iliyojegwa na kukarabatiwa kwa Kamati ya Afya ya Kituo. Ambapo kwa sasa kituo kina uwezo wa kufanya upasuaji kwa wajawazito wapatao 15 kwa siku na upasuaji mdogo mdogo kiwemo mabusha na hernia kwa wateja 30 kwa siku.
Tarehe 22/07/2017 saa 9:05 alfajiri Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Dr. Joseph Ligoha na Dr. Humphrey Masuki wakisirikiana na jopo la wataalam wa Kituo hicho walifanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza kwa mama mjamzito. Upasuajia ambao umenyika kwa mafanikio makubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga anatoa pongezi za dhati kwa wadau wote wa maendeleo waliofanikisha kutoaji huduma ya upasuaji katika kituo cha Afya Maramba, Pia anachukua fursa hii kuwaomba kuendelea kuchangia katika upajikanaji na uboreshaji wa huduma za afya.
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 755 443 326
Simu: +255 755 443 326
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017