Na: Nassoro Rashid
MDC Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Bi. Zahara Abdul Msangi ameendelea kusisitiza Kasi na Ubora katika utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu ya Shule za Msingi inayotekelezwa katika Vijiji mbalimbali kwenye Halmashauri kupitia fedha za Ruzuku toka serikali kuu.
Mkurugenzi huyo ameyazungumza hayo siku ya Jumamosi Agosti 12, 2023 wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo ambapo alitembelea kwenye vijiji na kata mbalimbali za wilaya ya Mkinga kukagua maendeleo na kasi ya ujenzi kwa kuongozana na Afisa Elimu Msingi na Injinia wa Majengo wa Wilaya.
Aidha katika ukaguzi huo Bi. Zahara amesisitiza miradi ikamilike kwa wakati huku akisema ubora wa miradi hiyo iendane na thamani ya fedha zinazotumika.
"Fedha hizi tulizoletewa ni nyingi sana, hivyo hatuna budi kutekeleza wajibu wetu ipasavyo ili kufikia matarajio ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kufikisha maendeleo kwa Wananchi wote hususan wanaoishi vijijini, tukitekeleza miradi hii kwa wakati na ubora uliokusudiwa Watoto wetu watasoma vizuri, watafaulu na hatimaye tutaijenga Mkinga imara yenye maendeleo makubwa". Alisema Bi. Zahara
Jumla ya fedha shilingi Bilioni 1.35 zilipokelewa kwa mwaka wa fedha 2022-2023 na Halmashauri kutekeleza miradi ya elimu msingi lengo ikiwa ni kujenga na kukarabati miundombinu hiyo ili kuimarisha na kuendeleza kasi ya maendeleo ya sekta ya elimu wilayani humo.
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 755 443 326
Simu: +255 755 443 326
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017