Na: Nassoro Rashid - Mkinga DC Habari
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga Ndugu Omari Mashaka leo Julai 4, 2024 ameungana na watumishi pamoja na Wananchi kufanya usafi katika kituo cha Afya Mkinga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma nchini.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Ndugu Mashaka amewapongeza wananchi pamoja na watumishi kwa kushiriki ipasavyo zoezi la usafi huku akielezea kuwa usafi ni sehemu ya maisha ya kila siku hivyo amewasihi kujenga utamaduni huo mara kwa mara.
"Niwapongeze na kuwashukuru kwa kushiriki katika zoezi hili lililojumuisha viongozi wa kijiji, kata, wananchi pamoja na watumishi, niwaombe jitihadi mlizozionesha hapa muendelee nazo, naamini kwa umoja wetu tutaendelea kuiweka mkinga safi na ya kupendeza zaidi". Alisema Ndugu Mashaka
Sambamba na hilo Kaimu Mkurugenzi huyo aliongoza kikao Julai 03, 2024 ambacho kililenga kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi kazini pamoja na kuhakikisha watumishi wanajisajili na kujaza mipango kazi katika Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (PEPMIS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
Maadhimisho haya yamekuwa yakiratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni ikiwa ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchí wanachama huadhimisha kwa kufanya kongamano na maonesho ya kazí mbalimbali kuhusu Utumishi wa Umma.
Kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni "Kuwezesha kwa Utumishi wa Umma Uliojikita kwa Umma wa Afrika ya Karne ya 21 lliyojumuishi na Inayostawi; Ni Safari ya Mafunzo na Mabadiliko ya Kiteknolojia".
#Kaziiendelee
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 755 443 326
Simu: +255 755 443 326
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017