Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Hassan Surumbu ametoa maelekezo hayo leo tarehe 18.10.2022 wakati akiwa kwenye Ziara yake ya Kikazi katika Kata ya Duga maforoni. mkuu wa Wilaya huyo amefanya ziara yake hiyo ikiwa ni katika utendaji kazi wake wa kawaida lengo likiwa ni kukutana na Wananchi na kuzungumza nao ili kuweza kufahamu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo Wananchi hao. sambamba na mkutano huo mkuu wa kijiji Mkuu wa Wilaya pia amekutana na Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu ambao ni wanufaika wa Asilimia 2% za mkopo unaotolewa na Halmashauri ili kuweza kutambua pia changamoto ambazo wanakutana nazo. kiongozi wa Walemavu hao alimuomba Mh mkuu wa Wilaya huyo kuhakikisha wanapatiwa Elimu ya Namna ya kufanya Marejesho kwa njia ya Mfumo Mpya kwani wao bado hawafahamu ili waweze kufanya Marejesho yao kwa urahisi. sambamba na hilo Mh. Mkuu wa Wilaya alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ndg Hassan Hassan kuhakikisha wananchi hao wanapatiwa Elimu hiyo haraka Iwezekanavyo.
Aidaha Mkuu wa Wilaya aliweza kutembelea Miradi Mblaimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Kata hiyo ambayo ni
Marabaada ya ukaguzi huo wa Miradi Mh. Mkuu wa Wilaya ametoa maagizo mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na wataalamu wake:-
Aidha amewataka vijana kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ili waweze kupatiwa Mkopo nafuu waweze kufanya biashara halali.
Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Shule mama ya sekongari Duga Maforoni.
Soko la Chakula Duga Maforoni
Mh. Mkuu wa Wilaya akikagua Vizimba vya Soko la Chakula Duga Maforoni
Kasera, Tanga -HorohoroRoad
Postal Address: P O Box 6005 Tanga
Simu: +255 755 443 326
Simu: +255 755 443 326
Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz
Mkinga dc @ 2017