• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mkinga District Council
Mkinga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Livestock and Fishary
      • Works and Fire Recure
      • Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari Mawasiliano na Uhusiano
      • Ugavi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Legal
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma wa Maji
    • Huduma ya Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Maktaba ya Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Matukio
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WA DALUNI WAASWA KUUPOKEA NA KUUSIMAMIA MRADI WA MAGEUZI TASNIA YA MAZIWA

Posted on: January 28th, 2026

Na: Nassoro Rashid – Mkinga

Wananchi wa Kijiji cha Kisiwani 'A', Kata ya Daluni wilayani Mkinga wamehimizwa kuupokea, kuumiliki na kuusimamia vyema Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuboresha maisha na kipato cha wafugaji.

Wito huo umetolewa na Afisa Mifugo wa Wilaya ya Mkinga, Ndugu Hosea Noel, wakati akiutambulisha mradi huo mbele ya wananchi wa kijiji hicho, akieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga imebahatika kuwa miongoni mwa halmashauri 21 pekee nchini zilizochaguliwa kunufaika na mradi huo kati ya halmashauri 184 zilizopo Tanzania Bara na Visiwani.

Amesema mradi huo uko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali, akilitaja Shirika la IFAD kuwa mhisani mkubwa, na kwamba utekelezaji wake utachukua muda wa miaka 10.

“Mradi huu unalenga kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya maziwa kuanzia uzalishaji, huduma za ugani hadi masoko na uchakataji wa maziwa, ili mfugaji aweze kunufaika moja kwa moja,” amesema Noel.

Amefafanua kuwa katika upande wa uzalishaji, mradi utahusisha ugawaji wa ng’ombe wa maziwa, mafunzo ya ufugaji bora, huduma za upandikizaji kwa chupa, upandaji na uhifadhi wa malisho kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa na kupata ng’ombe bora wenye tija.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, asilimia 20 ya wanufaika wa mradi italenga kaya zenye uhitaji mkubwa, ambapo watapatiwa ng’ombe mmoja wa maziwa bure pamoja na ujenzi wa banda na huduma nyingine muhimu.

“Lengo ni kumkwamua mwananchi aliyekuwa katika hali duni kabisa aweze kuinuka kiuchumi na angalau awe na uhakika wa chakula na kipato,” amesisitiza.

Ameonya kuwa uchaguzi wa wanufaika hao lazima ufanyike kwa uadilifu mkubwa kupitia Serikali ya Kijiji na Halmashauri, akibainisha kuwa dosari yoyote inaweza kusababisha mradi huo kuondolewa na kupelekwa eneo jingine.

Kwa upande wa asilimia 80 ya wafugaji waliobaki, amesema watanufaika kwa kuchangia asilimia 25 ya gharama ya ng’ombe kupitia utaratibu wa mkopo utakaowekwa wazi, huku akieleza kuwa mfumo wa “ndama wa kwanza jike kumpa mwingine” utatumika ili kuongeza idadi ya wanufaika katika jamii.

Aidha, amesema mradi utahakikisha upatikanaji wa huduma za uhakika za upandikizaji kwa chupa kwa kuwapatia vifaa wapandishaji wa wilaya, hatua itakayosaidia kupunguza matumizi ya madume duni na kuongeza uzalishaji wa maziwa bora.

Katika upande wa masoko, Noel amesema wahusika wa masoko watahusishwa kutafuta masoko ya uhakika kwa wafugaji, na pale itakapobainika hakuna soko la moja kwa moja, wafugaji watafundishwa uchakataji wa maziwa kuwa bidhaa mbalimbali kama maziwa ya mgando.

Akihitimisha, Afisa Mifugo huyo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo, akisisitiza kuwa miradi ya serikali hutathminiwa kwa matokeo, na endapo juhudi hazitaonekana, huondolewa.

“Mradi huu ni fursa adhimu kwa Wilaya ya Mkinga, tuupokee, tuulinde na tuhakikishe tunafikia malengo yake,” amesema.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA October 16, 2023
  • HATI MILIKI ZA ARDHI ZILIZOKAMILIKA WILAYA MKINGA December 04, 2022
  • KUSAFISHA MAENEO KWA WAMILIKI WA VIWANJA MKINGA August 12, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA July 18, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 23, 2025
  • MAKARANI WAOMNGOZAJI WAPIGA KURA WAASWA KUWA WAADILIFU

    October 25, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

Angalia zaidi

Kurasa za Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Habari

Kurasa Mashuhuri

  • OR- TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Salary slip portal
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Taifa
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Kasera, Tanga -HorohoroRoad

    Postal Address: P O Box 6005 Tanga

    Simu: +255 027-2660501

    Simu: +255 684 625 299

    Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Huduma

Mkinga dc @ 2017