• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mkinga District Council
Mkinga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Livestock and Fishary
      • Works and Fire Recure
      • Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari Mawasiliano na Uhusiano
      • Ugavi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Legal
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma wa Maji
    • Huduma ya Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Maktaba ya Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Matukio
    • Habari
    • Matukio

MTAALAMU AFICHUA FURSA KUBWA ZA MRADI WA MAGEUZI YA TASNIA YA MAZIWA YA MKINGA

Posted on: January 27th, 2026

Na: Nassoro Rashid

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea kutekeleza Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, unaolenga kuboresha uzalishaji wa maziwa na kuongeza kipato cha wananchi.

Akizungumza katika mahojiano, Mtaalamu wa masuala ya jamii kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndugu Charles Lugamala, amesema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo wakiongozwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), ukiwa ni mradi wa kimkakati wa kuleta mageuzi ya kweli katika sekta ya mifugo nchini.

“Huu ni mradi wa kimkakati wa Serikali unaolenga kuleta mageuzi makubwa katika tasnia ya maziwa nchini kwa kuzingatia uzalishaji wenye tija, uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza kipato cha wananchi,” amesema Lugamala.

Ameeleza kuwa mradi huo wa miaka 10 unatekelezwa katika mikoa 8 ya Tanzania Bara, ikiwemo Tanga, na kwa Mkoa wa Tanga unahusisha Halmashauri za Mkinga, Lushoto na Muheza. Mradi unatarajiwa kunufaisha jumla ya kaya 140,000, sawa na wanufaika wapatao 700,000 moja kwa moja.

Kwa mwaka wa kwanza wa utekelezaji, kaya 29,000 zinatarajiwa kuanza kunufaika, huku Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga ikitarajiwa kuwa na wanufaika wasiopungua 718.

Amefafanua kuwa mradi unatoa fursa katika maeneo makuu matatu ambayo ni uzalishaji, masoko na uratibu wa mradi. Katika uzalishaji, mradi unalenga kuboresha mbegu bora za mifugo, malisho, huduma za maji na tiba ya mifugo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa maziwa.

Kwa upande wa masoko, mradi utaimarisha mnyororo wa thamani wa maziwa kuanzia ukusanyaji, usindikaji hadi miundombinu ya usafirishaji, ikiwemo ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilometa 173 katika maeneo ya mradi.

Aidha, mradi utatoa fursa za kifedha ikiwemo mikopo yenye riba nafuu na kuimarisha ujasiriamali kwa wadau wa tasnia ya maziwa ili kuongeza uzalishaji na kipato cha wananchi.

Katika vipaumbele vya wanufaika, Lugamala amesema mradi umezingatia makundi yaliyoachwa nyuma kwa muda mrefu, hususan wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika fursa za kiuchumi zinazotokana na tasnia ya maziwa.

Kuhusu tukio la Mkinga, amesema uwepo wao ni kwa ajili ya kuzindua Jukwaa la Wadau wa Maziwa, linalowakutanisha wazalishaji, wasindikaji, taasisi za fedha, vyama vya ushirika na wadau wengine kwa lengo la kujadili fursa, changamoto na kuweka vipaumbele vya maendeleo ya tasnia ya maziwa kwa manufaa ya wananchi.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA October 16, 2023
  • HATI MILIKI ZA ARDHI ZILIZOKAMILIKA WILAYA MKINGA December 04, 2022
  • KUSAFISHA MAENEO KWA WAMILIKI WA VIWANJA MKINGA August 12, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA July 18, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 23, 2025
  • MAKARANI WAOMNGOZAJI WAPIGA KURA WAASWA KUWA WAADILIFU

    October 25, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

Angalia zaidi

Kurasa za Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Habari

Kurasa Mashuhuri

  • OR- TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Salary slip portal
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Taifa
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Kasera, Tanga -HorohoroRoad

    Postal Address: P O Box 6005 Tanga

    Simu: +255 027-2660501

    Simu: +255 684 625 299

    Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Huduma

Mkinga dc @ 2017