• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mkinga District Council
Mkinga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Livestock and Fishary
      • Works and Fire Recure
      • Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari Mawasiliano na Uhusiano
      • Ugavi
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Legal
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma wa Maji
    • Huduma ya Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Madiwani
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Maktaba ya Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Matukio
    • Habari
    • Matukio

MHE. MWAKIOJA: MIKOPO YA 10% NI NYENZO YA KUJIAJIRI NA KUPUNGUZA UMASIKINI

Posted on: December 24th, 2025

Na: Dominick Cosmas - Mkinga

Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Mhe. Twaha Said Mwakioja, amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuitumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujiajiri, kuongeza kipato na kuchangia kupunguza umaskini katika jamii.

Mhe. Mwakioja ameyasema hayo Desemba 23, 2025, wakati akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, akieleza kuwa kurejea kwa mikopo hiyo ni faraja kubwa kwa wananchi wa Mkinga baada ya kusimama kwa muda mwaka 2023 ili kuweka mifumo bora ya uwazi na ufanisi.

“Ni wajibu wetu sisi wana Mkinga kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kurejesha mikopo hii ambayo sasa inalenga kuwafikia wananchi kwa uwazi na kuleta tija halisi,” alisema Mbunge huyo.

Alieleza kuwa tangu kurejeshwa kwa mikopo hiyo mwaka 2024 na kuendelea mwaka 2025, zaidi ya shilingi milioni 546 zimetolewa kwa wananchi wa Mkinga pekee, fedha ambazo zimelenga makundi mbalimbali ya kijamii.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, vikundi 54 vya wanawake vimenufaika na mikopo yenye jumla ya zaidi ya shilingi milioni 290, huku vijana nao wakinufaika na zaidi ya shilingi milioni 247, akisisitiza kuwa mikopo hiyo haina riba na inalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Mbunge huyo alibainisha kuwa serikali haitoi mikopo hiyo kama sadaka bali kama chombo cha utekelezaji wa malengo makuu matatu; kwanza kuwawezesha wananchi kujiajiri na kuanzisha biashara zitakazozalisha ajira kwao na kwa wengine, pili kuongeza uzalishaji wa kipato ili kupunguza umaskini, na tatu kuwajengea wananchi utamaduni wa kushirikiana kupitia vikundi.

Ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara pamoja na watumishi wote wanaosimamia zoezi la utoaji na ufuatiliaji wa mikopo hiyo, kwa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia walengwa.

Tangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA October 16, 2023
  • HATI MILIKI ZA ARDHI ZILIZOKAMILIKA WILAYA MKINGA December 04, 2022
  • KUSAFISHA MAENEO KWA WAMILIKI WA VIWANJA MKINGA August 12, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA July 18, 2024
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UZALISHAJI WA CHAKULA

    October 16, 2025
  • WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 23, 2025
  • MAKARANI WAOMNGOZAJI WAPIGA KURA WAASWA KUWA WAADILIFU

    October 25, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

Angalia zaidi

Kurasa za Haraka

  • Fomu za Maombi
  • Habari

Kurasa Mashuhuri

  • OR- TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Salary slip portal
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Taifa
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Kasera, Tanga -HorohoroRoad

    Postal Address: P O Box 6005 Tanga

    Simu: +255 027-2660501

    Simu: +255 684 625 299

    Barua Pepe: Info@mkingadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Huduma

Mkinga dc @ 2017