Pichani ni Bi Catherine Mushi ambae pia ni Mwanasheria wa ABBOTT FUND TANZANIA akifafanua mada katika Mafunzo yanayoendelea yahusuyo Sheria kwa Washauri wa Kisheria Wilayani Mkinga , mafunzo hayo yamelenga kuwajengea Uwezo Washauri hao,
aidha mafunzo hayo yamelenga hasa kwenye upande wa kufahamu Haki za Msingi za Binadamu, Haki za Watoto , Ndoa , Mirathi, Wasia na Muundo wa Mahakama. lengo hasa la mafunzo haya ni kutatua migogoro kwa amani na kupunguza mrundikano wa kesi Mahakamani.
Mafunzo haya hutolewa Kila mwaka na kwa mwaka huu yatadumu kwa muda wa siku mbili yaani tarehe 2-3/5/2019. Pia mafunzo haya yanafadhiliwa na ABBOTT FUND TANZANIA.
Pichani aliekaa mbele ni Mratibu wa ABBOT FUND TANZANIA WILAYA MKINGA Bi Irene Mosha akizungumza jambo na wanufaika wa mafunzo hayo ambao ni Washauri wa Kiseria.
Kasera , Tanga-Horohoro Road
Postal Address: P.o.Box 6005 Tanga
Simu: +255 27 2977200
Simu: +255 684625299
Barua Pepe: info@mkingadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Mkinga .Haki zote zimehifadhiwa.